Shisia.
She's not your ordinary birthday girl. Not my ordinary. She's not the kind of person you just text, "HBD. TML. Or Happy Belated (for those who are always late😄)." NO. Not at all.
Shisia. She deserves a five, ten, fifteeen....pages of handwritten notes, letters.. whatever you might decide to call it. Fifteen pages just to say the least. And then have it delivered by a DOVE. Huh! 🕊 have a history of being good messengers. Remember the times of Noah? During the floods? Genesis 8:11 (KJV) And the dove came in to him in the evening; and, lo, in her mouth was an olive leaf pluckt off: so Noah knew that the waters were abated from off the earth. And so I will trust it.
Shisia deserves a poem. Written from the heart. But for today, I will do something sweeter...... a birthday blog sprinkled with love, much Swahili, and some French like pas de soucis (Copied from her about. No worries 😃). I know there's a language that will directly reach to her heart. That will talk to her in ways that I can't, but sadly I don't not know it. (I should probably take some few lessons to get closer to the polygot dream and best of it all, CLOSER TO HER HEART).
Shisia is a Neuroscience enthusiast. You will expect someone in neuro to be buried in books. Not so fun to be with or interact with. Or if so, then from a great distance. You will think she's incapable of banter. Wrong. Wrong. So wrong. Shisia will explain about the brain and nervous system, hormones starting from oxytocin to dopamine to serotonin. About neuroplasticity. She will about books. Challenge you about mothers and the role they play in both their husbands and children's life. About life and other societal matters. About doing things to God's glory. About salons, more so the Nairobi Salons. In short, about everything.
Leo nimeamua kutumia lugha yangu pendwa. Leo naandika kuhusu mengi lakini mhusika mkuu atakuwa Shisia. Shisia kutoka Kasarani. Ni mdogo kiasi kimwili lakini yale anayoweza kuyastahimili, kuyaelewa, kuyaeleza kamwe hayawezi kulinganishwa na chochote; yanaweza lakini. Nikijaribu nawezakusema nayalinganisha kama uzito wa nyota. Shisia ni binti ambaye ukiwa naye unahisi mtiririko wa upendo kwa njia spesheli. Ukijaribu kutabasamu, yeye anatabasamu mara mbili.
Ukicheka, yeye anacheka zaidi.
Nadhani ikiwa utaanguka, atakusaidia kuinuka pale awezapo. Anaweza pia kukaa chini na wewe kwanza, mbonge, mjue sababu ya kuanguka kwanza ndipo mengine yafuate.
Shisia aliingia maishani mwangu mwaka wa ishirini na mbili.('22) Tulikuwa katika birika birika za kujiandaa kujiunga na chuo kikuu. We were both floating in that weird post form four fog. Wakati ambapo umemaliza shule ya sekondari lakini ni kama bado maisha hayajaanza.... wakati ambapo wasiwasi pekee unayo ni, "Nitavaa nguo gani, Nitaitwa chuo kipi? When will kuccps open? Will my points be enough? How often should I go to church? Nitanunua sms za juma au mwezi? Data nitatumia ya safaricom ama airtel?...." Tulikutana. Tulitembea. Tulicheka pamoja. Tulikuwa na wakati wa masomo kama vile tulipovichanganua vitabu, Half of a Yellow Sun ikiwa moja yavyo, na kujitayarisha na mtihani wa SAT. (Huu mtihani huu!) Ulinipa wasiwasi. Kihoro cha moyo. Sikuwahijaribiwa hapo awali kwenye mtihani ambao uliihitaji muda mfupi zaidi. Standardized. (Lakini kwa yote, namshukuru Jalali aliwezakutufunza. Kuwa wepesi wa kufikiria na kutatua mambo. Sana sana tulipokuwa tukisoma fahamu za Kimombo na hakukuwepo muda wa kutosha kufikiria. Lazima ungebuni mwenyewe njia ya kuyajibu maswali kwa ufasaha na chini ya muda kidogo). Nilijifunza mengi kutokana na huu mtihani. Mengi ambayo yanasaidia kwa mitihani iliyofuata hata katika chuo kikuu. Imesaidia hata maishani. Haya kando. Hii si siku yangu. Ni siku ya binti Shisia.
Mnakumbuka zile hikes ambazo mnasema hapa lazima tujitayarishe kuhema, kupumzika, kusweat, kunywa maji mengi, kuchoka? Lakini bado mnapanda tu? Mnatembea tu? Yaani hiking na Shisia ilikuwa kama therapy. Pale Torok Falls. Najawa na tabasamu ninapoikumbuka. Akiwa amevaa shati lake jekundu na huku kiunoni kafunga sweta yake ya kijivu. Na ile laughter yake? Hee!
Kuna siku nyingine aliniwekea cornrows. Zilikuwa tight kidogo but tender. Nilipenda mwonekano wake. Watu wangedhani nilisongwa kwenye salon maaruf Eldoret. Zilikuwa nane(Haha!).
Wakati mmoja Shisia alinitumia waraka kutoka Providence. Waraka halisi haswa. Ulioandikwa kwa mkono. Mkono wake wa kulia nadhani. Hati safi na nadhifu. Haikuwa email. Hapana. Haikuwa DM. Nah. Wala haikuwa screenshot ya a quote kutoka Quora ama Pinterest. Ilikuwa waraka. Waraka halisi.
Yaliyonakiriwa:
Machozi yalinilenga kama maji ya mvua wa Julai na Novemba. Nilihisi kibaridi na kijoto intermittently. Nilikuwa pekee yangu kwenye jumbo langu. Nilijiuliza maswali kimoyomoyo. Nilijiongelesha. Ungedhani binti karopokwa. Nilijiambia, "Kidogo nilikuwa nimesahau mimi ni nani."
Tangia wakati huo nilijua kuwa Shisia hakukuwa rafiki tu. Ni yule akiona uwezo ama potential kwa lugha ya Kimombo anaisema. Anaona dhahabu pale wengine wanaoona vumbi (Wanaona dust sounds better..iykyk😄). Anapoangalia mtu anaona zaidi ya surface. Anaona nafsi. Anaona ndoto. Anaona MAAJABU (Hapa simaanishi yale maajabu ya Musa). Maajabu mazuri.
Wakati mwingi tulipokuwa tukipiga gumzo, lugha ya Kimombo ilishika usukani. Awali, Kiswahili ndiyo lugha iliyotawala. Kiingereza sounded fancier na hiyo ikakuwa chanzo cha kukihamia. Wee, "Ukinunua kipya usijaribu kutupa cha zamani." Kiliniramba kidogo.
Nilikuwa nimekosea. Lakini Kiswahili sasa narudi nyumbani. Nimetembea mbali nawe, SASA NARUDI. Nilipotelea Kimomboni nikidhani nitapata raha ya kweli. Narudi, narudi. Kutoka Kimomboni. Sasa unikaribishe. Nimepoteza saa, siku, miezi, na hata miaka. Naomba msamaha kwa kukuweka kando. Kwa kutofikiria nikikutumia. Nimechoka na Kimombo. Nimechoka kukitumia kila wasaa. Nakuaminia sana jinsi ninavyoaminia Ekegusii. Naamini umuhimu wako. Sasa narudi. Nimevunjika siwezi, Kiswahili. Nadai kupata nguvu mpya. Miiimii narudi!
Shisia alinikumbusha tena. Maneno yake yalikuwa yenye himizo kubwa. Ilikuwa Desemba tarehe ishirini na mbili. Ujumbe ulinifikia nikiwa nimetulia na kikombe cha chai na andazi mkononi. Ulikuwa mwanzo mtamu wa siku!
Nilianza kufikiria kwa Kiswahili tena. Nilimkumbuka Tamima, Bwana Maksuudi, Maimuna na wengine. Nilizikumbuka mbinu za uandishi kama vile matumizi ya barua na hadithi ndani ya hadithi. Nilitamani sana kuzitumia kwenye uandishi wangu. Hadithi kweli mbinu tamu. Nilikumbuka yale ambayo niliyahifadhi kwenye kumbukumbu. Kwa mfano mwandishi akinena, "Kijana mwenye sura ya kiume ya kuvutia. Mwenye siha. Weusi uliokoza. Kifua kikubwa, lakini kijana kakosa mguu." Maimuna alichagua kuwa naye. Kiapo cha kweli cha mapenzi kisichojificha nyuma ya hali ya mwili. Ni jambo la kufurahisha kupita maelezo. Ni nadra sana kupata binadamu wa hii hulka.
Maneno kama vile, "Nilikenua tu bila kunena kwa vile sikuwa na la kuamba. Nilipofungua mdomo kunena, mdomo ulianza kutetemeka," yalijikariri. Ni flex sana mtu kukumbuka yale aliyoyasoma miaka kadhaa iliyopita. Yanakufanya unatabasamu hasa unapojipata kwenye hizo situations. Sana sana kutetemeka unapozungumza. Kwa njia nzuri lakini.
Sehemu ya recollection yangu iliyonifikisha kwenye upeo wa furaha yangu ni ile ya,
Mhusika 1: Hautaki hela?
Mhusika 2: Nini hela mbele ya utu?
Mwandishi: Maneno yale kamwe hayakuwa ya kutania. Yalitoka kwenye dhati yake.
Si maneno unayo au utakayoyasikia kila siku. Nadra sana. Ni mara ngapi tumeeka hela mbele tukasahau utu? Kuna mengi zaidi ya hela. Utu. Utu ni wa maana.
Sehemu nilinakiri kwenye buku, "Siku hiyo niliimba taanusi njema. Hasa za mapenzi lakini kamwe hazikupeperusha kivuli cha Adrian." Ah! Adrian amekuwa muse wangu kwa miaka mingi sasa. Hayuko kwa maisha halisi. Ilikuwa furaha kuweza kuhusisha nyimbo na mtu fulani hata kama ni kwa fikira tu. Nyimbo zilizokuwa pendwa kwangu wakati ule si pendwa tena sasa hivi. Mengi yamebadilika lakini tunashukuru kwa zile enzi.
Mwendelezo wa niliyonakiri. "Lakini Adrian, uso wake, mtazamo wake, macho yake, ukarimu wake, kauli yake, vilikuwa alama ya kunipa kila uhakika kwa mwanamme." Utamu wa hadithi. Inakupa furaha mwenyewe. Unahisi ukitabasamu kiholela. Na hii? Hii iliyapa maisha yangu furaha ghaya. Ningehisi kuwa binadamu tena. Mwenye hisia. Mwenye furaha. Tena nilikuwa nimeanza kubaleghe.ðŸ¤
"Harusi ni jambo la furaha kwangu na kwako. Na ikiwa huwezi, basi usilie." Haya maneno yalilovya machozi kwenye chemchemi yangu. Zaidi zaidi. Nikifikiria sasa hivi, naona vile yanapasi lesoni muhimu kwenye vipengele mbalimbali vya maisha.
Hiki kisengerenyuma kinanikumbusha mbali. Miaka tisa imepita. Moyo wangu umejaa hisia zisizoeleweka. Machozi yananiranda kwelikweli. Nafsi yangu imenyamazishwa na mshikamano wa matumaini. Ndani yangu kuna nguvu inayonisukuma niendelee kuandika.
Nimejivuta machozi. Lazima niendelee kuandika.
Mmoja wa wahusika ambaye jina kidogo limepotea alisema, "Ikiwa ipo njia ya kurekebisha dosari, ifanye." Alitambua makosa kuwa fursa ya ukuaji. Mzungumziwa alikuwa na maisha kabla. Best said in English, 'a past.' Lakini bado aliamua kumkubali kwa yote. Kulikuwa na eneo salama (Direct translation of safe space, huhu!). Ambalo lilisema yes Okeromi, yes Nyabuto(wahusika wa kubuni), yes, yes......nimekusikia, lakini kama bado unawezakurekebisha yale uliyofanya, kamwe USISITE. Tamu sana.
Ukurasa baada ya mwingine, niliyasoma mengi. Mengi sana. Kisha nikafika mahali ambapo mhusika alisema, "Uanaume wangu hautiwi doa na niliyoyatenda zamani; ndiyo umeshayafanya. Mimi sihusiki na ya zamani. Nahusika na ya sasa. Hoja masikilizano." Maneno haya yalinifanya nikae kimya. Kimya chenye tafakuri nzito. Niliyasoma tena. Na tena. Niliyanakiri kwenye buku. Kwa sababu ni vigumu kupata roho inayojielewa kiasi hicho. Ambayo inakiri kilichotokea. Na bado inatamani mguso wa neema ya kuyachuchumia ya mbele.😊
Na hapo ndipo nilipomwona Mungu. Katika nafasi hii ndogo. Ni Mungu yule anayesema, "Tazama, nayafanya yote kuwa mapya." (Ufunuo 21:5). Maneno haya yalinikumbusha kuwa, hata mtu aliyetanga mbali na kweli, bado anaweza kuwa chombo kipya cha heshima mikononi mwa Bwana. How sweet.😋
Kama bado sijamaliza kukisoma kitabu, niliisikia sauti ya bibi yangu ikiniita. Laini, ya upole, lakini yenye uzito wa kumbukumbu nyingi.
“Faith... Faith...”
Nilijibu kwa sauti ya kike kabisa, ile sauti ambayo haijabadilishwa na dunia. Ambayo imetunzwa na upendo wa nyumbani (Love at home.)❤️
“Naam!” "Eeee" kwa mwitiko wa nyumbani.
Nikiwa bado nimekaa chini, juu ya leso ile ile aliyokuwa amenipokeza nilipokuwa mdogo yenye rangi ya samawati iliyochakaa kwa heshima ya miaka, nikajikuta nikipata pumziko.
Pepo laini ilipita. Iliambatana na harufu ya udongo kutokana na mvua iliyokuwa imenyesha siku mbili awali. Niliinusa harufu ya zamani ya leso. Harufu ya sabuni menengai na omo. Harufu ya mikono ya bibi.
Nilishikilia kitabu kwa mkono mmoja na leso mkono mwingine. Teketeke nilikuwa tayari kwenye mlango wa nyumba mahali sauti ya bibi ilitoka.
Baada ya kumaliza shughuli niliyoitiwa, nilirudi kitabuni. Nilikuwa nimetulia kidogo. Niliketi tena juu ya ile leso, nikaisahihisha. Majani ya mpera yaliendelea kuanguka. Upepo uliendelea kuvuma. Ulikuwa mwanana.
Nikafungua ukurasa ule ule niliouachia.
Na hapo ndipo nikakumbana na dondoo ya mwisho nitakayonakiri kwenye masimulizi yangu ya leo:
"Kila siku sadfa hutuingia na kuturudisha tunakokimbia, na kutukutanisha tusipotazamia." Niliisoma mara mbili. Mara tatu. Hayakuwa maandishi tena. Ilikuwa sauti. Sauti ya maisha. Sauti ya Mungu. Niliketi pale kwa muda, macho yakiangalia mbali. Sadfa inayotufunza kwamba hakuna pa kukimbilia zaidi ya ukwelini, zaidi ya kwake. Na kuna wakati pia, sadfa hukutana nawe pale haukutumainia katu. Kama unapokumbana na mtu, au maneno, au kumbukumbu, ambayo haukutarajia lakini ilikusudiwa na mbingu.
Niliufunga ukurasa huo polepole na kuendelea.
Nilimaliza kusoma Utengano Desemba tarehe nane. Ni hadithi iliyonigusa kwa undani. Kurasa za mwisho ziliniliza na pia zilinifurahisha kwa njia isiyoweza kueleweka kirahisi. Nililovya si kwa huzuni tu ya yaliyotokea kwa wahusika, bali kwa uzuri wa namna ambavyo mwandishi alivyopanga maneno. Kwa uchungu, upendo, na ukweli.
Nilikaa kimya kwa dakika kadhaa. Nilikishika kitabu na kukikumbatia kifuani mwangu. Kumbatio la kweli. Nilihisi kama nilikuwa nimetembea ndani ya maisha ya wahusika, nikaona mapambano yao, na tumaini la nuru baada ya giza. Kwa yote, moyo wangu ulijawa na shukrani.
Nitakisoma tena na tena. Kwangu utengano si riwaya tu. Ni mwalimu wa dhati na wa moyoni.
Lesoni nilizosoma:
I'm so thankful to God for those who have mastered the art of using words in a way that brings so much joy. In a way that teaches life lessons that are remembered long after. Lessons that are there to stay. Live long authors? Writers? Poets? Live long. I mean this.
Nimetanga.😄 Kweli nimetanga. I have wandered. Niliweka nia kuwa Shisia leo ndiye angekuwa kitovu cha masimulizi ya leo. Lakini pia, singeweza kabisa kuondoka kimya kimya bila kuwatupia uhondo kidogo. Angalau mpate kuonja kile nilichoonja.
Subiri kwanza. Kumbe nilikuwa nimemsahau mhusika mkuu.
Picha hii:
Anaonekana hapo, akiwa amevaa sketi nyeupe inayoweza kuyumbishwa kwa upepo wa jioni, safi kama ukurasa wa mwanzo wa simulizi langu.T-shati ya rangi ya chungwa imekolea mwanga wa machweo. Rasta zake za kahawia zimejipanga kwa utulivu kama mistari ya mkono unaondika. Mkono unaopenda kuandika. Sauti yangu ya ndani inanong’ona, “Shisia ndiye huyu. Vipi ulimsahau?"
Na sasa, mkono unajikunja polepole. Tayari kuendelea kumwandikia Shisia.
Yeye kuongelelea kuhusu Swahili stories ilinikumbusha kuhusu Utengano na riwaya nyingine ikiwemo Chozi la Heri (My highschool sweetheart). Maybe bila yeye bado ningekuwa na captions za Kimombo tu. Kama, "Grace has led me this far, and it will lead me home." Swahili inafurahisha hata kama yote ina maana sawa. Eti, " Neema imenileta huu umbali, na bila shaka, itanifikisha nyumbani." 🤗
Mimi na Kifaransa hatukuwa wendani. Hii lugha ilikuwa inakaa tongue twister. Nilisema hii kwa kweli si yangu kujua. Ina wake. Shisia akiwa mmojawao. Niliona status zake. Nyingine zilizoandikwa kwa Kifaransa. Na nyingine akizungumza. Niliifurahishwa. Nikawa na hamu ya kujua na zaidi ya yote kuzungumza. Nilijiambia, "Mimi pia naweza kuyaelewa maneno ya Kifaransa na kuzungumza kwa ufasaha." Nikadownload Duolingo. Nilianza na misamiati rahisi kama vile, "Bonjour, Como ca va, bien, uno, deux...." Msingi tu na hii ilitosheleza roho yangu sana. Niliandika yale niliyoyajua kwenye buku mara kadhaa. Wacha tu.
Shisia alianzisha huu mto bila kujua na Mungu akaongeza moto wa kufahamu. Mungu ni mwema. Siku zote.
Tulitengana. Kila mmoja akaenda zake. Tulidumisha mawasiliano kupitia kwa mtandao. Heri nusu shari. Ama?
Tulikutana tena Januari elfu mbili ishirini na nne. Katika mazingira tofauti na ya nyumbani. Nilifurahi kumwona na kusikia jinsi maisha yalivyompeleka katika nchi ya ugenini. Tulicheka pamoja huku tukila mapocho. Kwa mapocho namaanisha Ugali, Chapati, na vyakula vingine vya nyumbani. Tulijihisi kuwa nyumbani mbali na nyumbani. Tulikula, tukanywa, tukashiba. Tulikunywa hasa maji. Baadae kutakutana tena na marafiki na wenzetu. Tulisikiliza nyimbo zilizopendwa. Tenzi za rohoni za zamani na za kisasa. Tulipiga picha na kuchukua video. Wendani wangu na wenzetu: Mercy(aka Kitimbakwiri), Halima, Moha, Edu, Vee, Vinny, Tat, Starlone na wengine walikuwa baadhi ya waliohudhuria. Nitadanganya nikisema sikuwa na furaha. Nilihisi kama mwanamke aliyekuwa amengoja miaka tano, kumi bila mtoto na baadae kujifungua mapacha. (Ni furaha ya kweli badaa ya athari kutoka kwa wakwe, marafiki, majirani, wanakijiji, na hata bwana mwenyewe).
Sad were the parting moments. Lakini ni nzuri tena kwa sababu inakupa hamu na tumaini la kukutana tena. Nilienda nikiwaza marafiki zangu na yale tuliyoshiriki pamoja kwayo.
Jalali ni mwema.
Machi ishirini na nane, '25, tulikutana tena na Shisia. Ah, muda ulikuwa umejaza mengi. Hatimaye, nyuso zetu zilijumuika tena.
Ilikuwa msimu wa baridi. Baridi ya kutufanya tukumbatie makoti mazito. Tulikuwa na wakati mzuri. Si kwa sababu kila kitu kilikuwa kamili, bali kwa sababu tulikuwa pamoja. Tuliinua macho yetu tukacheka. Wakati mwingine tuligawana kimya kidogo. Kwenye baridi hiyo, tulikula viazi vilivyochemshwa, ambavyo kusema ukweli havikuwa ladha tuliyoitamani. Ila hiyo haikuwa sababu yetu kutovila kwa sababu vilikuwa alama ya kushiriki. Asante kwa zile ndizi alizokuwa nazo Shisia. Zilileta furaha ya ziada kwenye mkate wetu wa mazungumzo. Zilitufanya tukumbuke kwamba hata vitu vidogo vinaweza kuleta furaha. Tulipiga gumzo. Kuhusu shule. Utofauti wa maisha humu na nyumbani. Hali ya siku kuyoyoma. Neema ya Mungu iliyotukutanisha tena. Tuliongelelea mambo tofauti tofauti. Pamoja tulihimizana. Tukapata motisha ya safari. Ni wakati wa kukumbuka. Lakini muda nao ni gani? Ulikuwa unaenda kwa kasi ingine sikuelewa. Bado tulikuwa na mengi ya kuzungumzia. Muda ulivaa sura ya kazi. Lazima tungeagana.
Moja kwa moja tulienda hadi stesheni ya treni. Tukapanda treni. Tulikaa karibu, Shisia na mimi, tukaendelea na mazungumzo yetu.
Hii picha tulipiga humo humo ndani ya treni.
Ni picha tu lakini ina kelele ya kumbukumbu.😊
Shisia alitoka mbele yangu, na tukaagana.
Salamu haikuwa ndefu, lakini ilikuwa kamili. Mioyoni tulijua: “Tutakutana tena. Maisha yanajua jinsi ya kuleta marafiki pamoja tena kwa wakati.” Pengine tutatabasamu kwenye reli nyingine, siku nyingine.
Shisia.
Free spirit? Check
Brains and beauty? Double check.
Someone who will make you laugh until your stomach hurts? Tripple check.
You will think I am writing for someone who has everything in place. No. The beauty is, Shisia is still blooming.🔥 Still discovering herself. Still becoming. Still blossoming.🌸 🌼 And that is what I admire her for. She's not perfect. But she's a symphony in progress. A work in progress. I love her for being her.
Kwa kila anayesoma haya, chukua muda mwambie rafiki yako kuwa unamthamini. Tuwafikirie na kuwashukuru wale wote wanaotupa sababu ya kutabasamu.
Neema ziwatiririkie.
🎉 Heri ya kuzaliwa, mpendwa.💛
Lovingly,
Mwango.💫
Msomaji miye ni Shisia😂. Nabubujikwa na furaha riboribo❤️🥹. How beautiful it is to experience you Faith. This means a lot. I am renewed to take on life with so much hope, courage... I didn't know how much my words meant to you.
ReplyDeleteAnd to even illustrate my feelings: I feel like I have dipped these long fingers of mine in this rich butter of love from you my friend and I'm just smothering myself in it😂. And it's making glow and feel so confident. Nashukuru
I have not read the whole thing, but sometimes I think someone can love another too much. But that is alright.
DeleteThis is so beautiful❤❤so heart warming how your friendship is deeply filled with love and appreciation. It feels so good to see girl friendships blossom. Happy birthday to Shisia.
ReplyDeleteOh, how she writes.
ReplyDeleteYou're such a lover girl Mwango, so happy to call you a friend. A confidant. With you I can always be myself. ❤️
Nafurahi kuwa umekifufua Kiswahili. Our Swahili holic pale Nyabu. Zidi kubarikiwa.
Wow!This is lovely ❤️ I just love seeing good friendships blossom🌸
ReplyDeleteGive us a book now, Mwango.🤗
ReplyDeleteGood friendship is built with resilient. ♥️♥️am happy with this kind of friendship. All that you people shared was amazing moments. May God keep you strong for one another. 🎉🎉Cheers Mwango🎉🎉
ReplyDeleteA yes will be the best balance, the future is very unknown, the weather changes and the wind breaks the silence and whistles amongst the trees. Kudos and cheers Mwango🎉
ReplyDelete